UJASIRIAMALI

Fikira Ambazo Hutakiwi kuwa nazo unapoanza UJASIRIAMALI.

Zipo fikira nyingi ambazo watu wanaotaka kuanzisha harakati za ujasiriamali hujikuta wakiwa nazo. Ukweli ni kwamba zingine ni sahihi na baadhi sio sahihi kabisa na huwa ni kikwazo kwa Wajasiriamali wanaochipukia.

Hebu tafakari na fikiri kidogo kuhusu hii misemo ambayo mara nyingi ipo ktk jamii yetu:-
1. Mwanzo mgumu.
2."Nataka niwe kama Bakhresa"
3. Matajiri wa Tanzania ni mafisadi tu.
4. "Dah! Ningekuwa na mtaji ningeanzisha biashara yangu."
5. "Mjini kuna fursa nyingi, si kama kijijini"
6. "Nipo nafanya mishe mishe tu, si unajua tena mtaani"
7. Kupanga ni kuchagua
8. "Maisha ni kombolela, butua uwaokoe wenzako."
9. Chezea mshahara, usichezee kazi
10. Iga kazi..., usiige matumizi,.... utaumbuka.

Je, wewe ni msemo gani unaoujua? Tafadhali comment msemo wako sasa ili tuje tuujadili zaidi.

Leo nataka nikufikirishe kuhusu jambo hili

"Tambua kwamba hautawezi kuwa kama mtu fulani katika jambo unalotaka kulifanya, kwa hiyo kamwe katika ujasiriamali usitafute kuwa kama fulani."Au wanasema, "You will never be like someone, you are unique", "Yes, you are who you are, never try to be like someone"


Haya maneno yana maana pana sana, si kwamba Mjasiriamali hatakiwi kuwa na "Mentor" wake, La Hasha!, namaanisha kwamba kila mtu ana nafasi ya kufikia malengo kwa mchanganyiko wa njia tofauti tofauti. changamoto zitakazokuwa katika biashara yako hazitafanana na za yule "Mentor" wako. Usijaribu ku "copy" kila kitu kutoka kwa mtu fulani hata kama alishafanikiwa sana. kuna mambo ya ndani ambayo mtu yeyote aliyekwishafanikiwa huwa hayaweki wazi katika jamii. Ataishia kusema, mimi nilianza tu taratibu na kazi fulani, nikawa kwa kweli nafanya bidii sana mfano wkt mwingine nililala kwa masaa matatu tu kwa siku kwa sababu ya majukumu. Lakini nikuulize swali, ukilala mda mchache katika ujasiriamali unaotaka kuuanzisha au uliokwisha kuuanza ndio utamfikia siku moja?!!!!!
Mambo ambayo yanafanya wewe usiwe sawa na mtu mwingine hata siku moja katika Ujasiriamali ni kama:-
1. Mpo katika mazingira tofauti
2. Alianza biashara katika kipindi tofauti na wewe, kumbuka vipindi havifanani kamwe.
3. Inawezekana pia mnafanya Ujasiriamali tofauti.
4. Yeye anazungukwa na watu tofauti na wale wanaokuzunguka.
5. Asili yenu, elimu na vipaji vyenu vinatofautiana.

Maada itaendelea, 
Karibu kwa maoni zaidi:
biragipaul@gmail.com, +255 758 162 447

BUSIMINET COMPANY LIMITED
busiminet@gmail.com, +255 765 901 093

Mwananyala-msikitini, Dar es salaam
Tunatoa huduma mbalimbali ukiwemo ushauri wa kibiashara pia.
Find us on facebook, blog and Jamii Forum .



1 comment: